Mambo Shamim,
Kusema kweli nimekua ni mdau mkubwa sana wa blog yako hata nikawa mmoja wa watoaji comments kwa watu mbalimbali wanaoomba msaada kupitia blog yakoSijajua ushauri wetu huwa unawork namna gani but nimeona nami leo niombe ushauri
Mimi nna miaka 27, sijui msichana sijui mwanamke, sijui nijiite mtu mzima lakini huo ndo umri wangu. Kwa sasanipo Nairobi kwa kazi fulani iliyoniweka huku kwa mwaka mmoja hivi kazi ambayo naimaliza na kurudi TZ next week moja kwa moja
Sasa shida yangu ni kwamba toka niingie Pubety nimekuwa na chunusi mpaka leo,imagine huo umri wangu then nilianza period yangu ya kwanza nikiwa na miaka 15 all this time nimekuwa na chunusi hazijawahi isha
Nimetumia cream za kawaida hizi sijui Princess na Persal kwa muda mrefu but In Vain
Mwaka juzi nikahamia kwenye Carolight mpaka mwa huu January, kusema kweli chunusi haziniishi zaidi ya kunibadilisha rangi ya ngozi, mi ni maji ya kunde
But nilivyofika huku nikaanza kutumia bidhaa za oriflame ambazo kusema kweli zimenirudisha kwenye ngozi yangu but chunusi zipo palepale, but kabla ya hapo niliendaga kwenye clinic fulani hiv pale Kwa Remi wanatoa dawa fulani hivi kama maji nilizitumia kama miezi mitatu hivi niliona naibiwa tu kwani hazikuisha na nilispenda kama laki nne hivi coz dawa zao ni expensive na wanatoa midawa kibao
Ila mpaka sasa natumia Oriflame products sema lakini bado ninazo tu, sina chunusi sana ila madoa ndo magumu kutoka, honestly ukiangalia ngozi yangu ya miguu unaweza usiamini kama usoni nipo na chunusi coz nina miguu softiiii
Nimeshafanya skin test na farbek, hata huku hawa oriflame walinifanyia waniambia kuwa nina mafuta mengi na juzi tu nimepima Agha Khan nimeambiwa nna mafuta mengi
Sasa kusema kweli siogopi itakua shingi ngapi coz nimetumia zaid ya hata sijui milioni ngapi toka nianze kutafuta suluhisho hili bila mafanikio so kama kuna mtu anayejua mahali ambapo kwa kweli nikienda ntapata tiba na kuisha ntashukuru nimechoka mwenzenu nadhani unajua chunusi zinavyofanya mtu kuwa unconfortable especially kama ni mtu wa kisasa
Unaweza angalia kwenye facebook picha zangu ukaona michunusi yangu kweli imenichosha...
mwalimmissie@yahoo.com
kama kuna mtu anaweza nitumia email kunielekeza but naomba ziwe ni sehemu ambazo kweli ntapata msaada staki chochote chenye SIDE-EFFECT mbaya kama kuchubua
Nitashukuru sana
Keep Rolling Mama...fans wako tunaendelea kukupa support
Thanks