Tuesday, November 23, 2010

MSHAURINI!!!

Naomba unisaidie na hata ukiwashirikisha wadau pia ni sawa (keep ma email plz)
Nina tatizo la makovu katika mwili wangu ukiacha spots za usoni shauri ya chunusi pia niliwahi kuugua tetekuanga nikiwa  mtoto(miaka kama 14+ sikumbuki vizuri).
Hii iliniacha na mabaka mengi hasa pande za miguuni hadi mapajani. Hali hii inanikosesha raha sana kiasi nashindwa kuvaa nguo fupi na nahisi kupitwa na fasheni kwani sasa nina umri (28yrs) so u can imagine navyotamani kuvaa at least nguo ya kufika magotini lakini nashindwa.
Namshukuru mungu nimeolewa ila sometimes nashindwa hata kumvalia mume wangu vile vivazi vyetu vya mitego mana nahisi kama atabaki kunishangaa kwani nahisi sivutii.
Ombi langu ni kama naweza pata dawa au kitu chachote kitachoweza kunisaidia kutoa kabisa haya makovu jamani. (Ila isinichubue )Nna mguu mzuri mashaalah ila ndo hivyo nashindwa kujinafasi.
tafadhali da Shamimu nisaidie.
Asante sana.
Wako mdau ,P.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...